6 Novemba 2024 - 16:42
Ushindi wa wawakilishi 2 wa Wanawake Waislamu wa Congress ya Amerika

"Rashidah Talib" na "Ilhan Omar", ambao walikuwa Wanawake wa kwanza wa Kiislamu na Kidemokrasia kuingia katika Bunge la Congress la Marekani, kwa mara nyingine tena wameshinda katika uchaguzi huu dhidi ya Wapinzani wao wa Chama cha Republican.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - "Rashidah Talib" na "Ilhan Omar", ambao walikuwa Wanawake wa kwanza wa Kiislamu na wa Kidemokrasia kuchaguliwa katika Bunge la Congress la Marekani, wameshinda tena katika uchaguzi huu dhidi ya wapinzani wao wa Chama cha Republican.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kanali ya Televisheni ya Al_Jazeera, Rashidah Talib, Mwanamke wa Kipalestina wa Bunge la Marekani, amechaguliwa kuwa Mwakilishi wa Jimbo hili katika Baraza la Wawakilishi la Marekani jana, Jumanne, kwa kuungwa mkono na Jumuiya kubwa ya Waarabu Wamarekani katika jimbo la Michigan.

Pia Ilhan Omar, akiwa kama Msomali Mmarekani, anaketi kwa mara nyingine tena katika Kiti cha Congress kwa muhula wa tatu huko Minnesota.

Taib, alikuwa mmoja wa wakosoaji Wakuu wa Uungaji mkono wa Kijeshi wa Marekani kwa Israeli katika vita na Gaza, na katika uchaguzi wa awali, alimshinda mpinzani wake wa Republican, James Hooper, na kuwakilisha Wilaya ya Kidemokrasia ya Kamala katika miji miwili ya "Dearborn" na "Detroit" katika jimbo la Michigan.

Omar, ni mkosoaji mwingine wa Israel katika vita vya Gaza, pia aliwashukuru wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii wakati wa kampeni, na aliandika hivi:

"Jitihada zetu ngumu zilistahili. Huu ni ushindi kwa sisi sote tunaoamini kuwa maisha bora ya baadaye yanawezekana. Siwezi kusubiri kuacha kujivunia kwa sababu yenu kwa miaka miwili ijayo."